MGODI WA BUZWAGI WAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA KAMA MALIPO YA HUDUMA.

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi madarasa ya shule ya msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi
Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma. 
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Kahama wakishuhudia makabidhiano hayo.




Mgodi wa Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
 
Akizungumzia malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.
Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.
“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata, ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post