Ticker

6/recent/ticker-posts

WALALIMU WA ARUSHA WACHARUKA



 Chama cha walimu mkoa wa Arusha waitisha maandamano ya waalimu yasiyo na kikomo kupinga uonevu wa walimu wanaotuhumiwa na wanafunzi hewa jijini Arusha 

Andrew Nazu ambaye ni Kaimu mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Arusha amesema, chama kimetoa siku 10 kwa Mkurugenzi wa jiji kufuta barua zilizowavua madaraka walimu 23 na waratibu wa Elimu kata kumi 

Wamesema hawatakubali kukaa meza moja na Mkurugenzi wa jiji mpaka pale watapowasikiliza madai ya walimu wanaotuhumiwa kuhusika na wanafunzi hewa 

"Tumegundua zoezi hili la uhakiki wa wanafunzi hewa na upatikanaji wa wanafunzi hewa kwa jiji umekuwa wa kionevu na tunao ushaidi , "alisema Kaimu mwenyekiti 

" Adhabu imetolewa bila kuwashirikisha chama wa walimu ama kamati ya walimu na pia hata hao walimu hawajapewa muda wa kusikilizwa, "alisema Kaimu

"Mkurugenzi alipigiwa simu kuwa asiwavue madaraka walimu mpaka watakapowasikiliza lakini hakufanya hivyo ,alikaidi na kuwavua madaraka ,tunasema atengue barua hizo ,"alisema Kaimu

Kwa upande wake Kaimu Katibu Nurueli Kavishe, amesema maandamano haya yatakuwa ya namna yake lengo likiwa ni kuhakikisha wanatetea uonevu unaofanywa na baadhi ya watu kisa ikiwa ni migogoro baina ya watu na watu na wengine wakifanya uonevu huo kwa lengo la kuweka watu wao kwenye nafasi hivyo

"Sisi hatutaogopa kupigwa na polisi ,tunasema polisi waandae mabomu na risasi lazima tuandamane ,"alisema Nuruel

Upande wa Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Arumeru Jocye Kizaji, amemtaja afisa elimu wa msingi wa jiji Hussen Mgewa kuwa moja wa maafisa waliokuwa mwiba kwa waalimu hasa akiwa ni mwenye kutoa lugha chafu kwa waalimu na kupelekea waalimu kudharaulika mitaani

"Huyu Afisa amekuwa mfano mbaya kwakutoa lugha chafu na yote tumeyarekodi maneno machafu aliyokuwa anawatolea walimu ,"alisema Jocye Kijazi

"Mimi nashanga kuna shule mwalimu hajapewa barua ya kushushwa madaraka ila mratibu kapewa na kisa ni mwanafunzi hewa moja,hapo haki iko wapi?alisema Jocye

Hata hivyo amewataka walimu wa halmashauri ya jiji ya arusha kuunga mkono maandamano hayo kutetea haki ya walimu walionewa




Post a Comment

0 Comments