Vijana nchini wapewa elimu kuhusu kujihusisha na shughuli za maendeleo
Kuelekea kilele cha siku ya vijana duniani, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja na kupewa elimu jinsi wanavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha pamoja na kukamilisha Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Christine Mwanukuzi-Kwayu, aliwataka vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kusaidia kubadilisha maisha yao binafsi na kwa taifa.
Mgeni rsmi katika kongamano hilo Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Christine Mwanukuzi-Kwayu akizungumza na vijana.
Alisema vijana wengi wamekuwa hawajihusishi na mambo ya maendeleo na hivyo ni wasaa sasa na wao waanze kujihusisha ili waweze kuchangia kuleta maendeleo katika taifa kwani hata takwimu kwa sasa zinaonyesha vijana wanashiriki kwa kiasi kidogo kutokana na wengi wao kutokuwa na ujuzi.
"Vijana hivi mnajua kama nyie ndiyo mnatarajiwa kuongoza taifa lakini bado mmelala hata katika uchunguzi uliofanyika unaonyesha vijana asilimia nne ndiyo wanajihusisha kwa karibu na shughuli za maendeleo kwa nchi yetu ila wengi mnakuwa hmajui," alisema Mwanukuzi-Kwayu.
Nae Meneja Miradi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro amesema kuwa matatizo wanayoyapata vijana duniani yanatokana na kutokua na ushirikishwaji wa vijana katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika nchi.
Meneja Miradi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro akiwapa vijana njia za kupata mafanikio na kuwaeleza mambo ambayo yanachangia wao kushindwa kufikia malengo.
“Changamoto zinazomkabili kijana nchini Tanzania ndio hizo hizo zinazoweza kumkabili kijana nchi nyingine, lakini haya yote hutokana na kutoshirikishwa kwa vijana katika sekta mbalimbali za uzaliashji na za kimaendeleo chini,” alisema Oscar
Na Hashimu Ibrahim
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa burudani kwa vijana waliohudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya vijana waliohudhuria kongamano hilo.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.