RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA ARUSHA FILEX NTIBENDA ,AMTEUWA MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA



Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na
Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake
umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako
atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es
Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post