Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya warembo 13 kutoka mikoa minne ya Kanda ya
kaskazini Jana wameingia rasmi kambini kwa ajili ya kujiandaa katika
shindano la kumtafuta mlibwende Wa kanda ya kaskazini.
Akizungumza na waandishi Wa Habari muandaaji Wa shindano
hilo Mkurugenzi Wa kampuni ya mwandago investment Faustin Mwandago
alisema teari maandalizi yote yamekamilika na warembo wote 13 kutoka
mikoa ya Arusha ,Manyara, Kilimanjaro na Tanga wameshaingia kambini kwa
ajili ya kujiandaa na shindano hilo.
Alisema kuwa anauwakika kabisa taji la mrembo Wa Tanzania
ambalo adi sasa bado linashikiliwa na mrembo kutoka kanda ya kaskazini
mkoani Arusha Lilian Kamazima watalitetea na litabaki kwakuwa warembo
wake ni wazuri na wanajiamini vyakutosha pamoja na nithamu ya hali ya
juu.
Alisema pia katika shindano la mwaka huu wamechagua warembo
ambao wanauelewa wa kutosha na wanajitambua hivyo wanaamini kabisa taji
litabaki kanda ya kaskazini.
"Mashindano ya mwaka huu ni tofauti na shindano hili
nilakipekee kwani tumeboresha mambo mengi sana kuanzia burudani ,warembo
wenye na hata ulinzi tumeweka historia ya kutoa miss Tanzania na
aitaishia apo tutaendelea kuwatoa warembo kanda hii mpaka watu wachoke
maana kanda ya kaskazini inawasichana wazuri wenyesifa zote za kuchukua
hili taji "alisema Mwandago.
Aidha alibainisha kuwa warembo watakaa kambini kwa muda Wa
siku sita adi Siku ya Augast 6 pale shindano hili litakapo fanyika
katika viwanja vya ukumbi Wa triple A Jijini hapa.
Alibainisha kuwa katika shindano hili la kumsaka mrembo Wa
kanda ya kaskazini(miss kanda ya kaskazini)bendi ya Fm Academia
inatarajiwa kutoa burudani ambapo alisema kuwa bendi hiyo imejipanga
kuwapagawisha washabiki wake kwakuwa burudani safi pamoja na staili mpya
za bendi hiyo.
Alitaja wathamini waliothamini onyesho hilo hadi sasa kuwa
ni clous view hotel ,Geo Security 'Mery saloon ,libeneke la kaskazini
blog,Triple A fm pamoja na mwandago investiment .
Aliongeza kwa kuzitaka kampuni mbalimbali kujitokeza kuzathamini shindano hili kwani nafasi bado zipo .
Alitaja viingilio vya onyesho hilo kuwa V.I.P itakuwa shilingi elfu 30000 huku kawaida ikiwa shilingi 10000.