Mkuu
wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiwapa vifaa tiba na madawa vilivyotolewa
na mdau wa maendeleo MKwawa Hunting safaris kwa zahanati ya Kitisi.
Vifaa na madawa vina thamani ya Shilingi Milioni 3. Kumekuwa na upungufu
wa madawa hapo zahanati ambapo wananchi walipata tabu.
Mkwawa Hunting safaris pia walitoa Shilingi milion 5
kwa ajili ya maendelea ya kijiji na hapo nyuma walishiriki ujenzi wa
nyumba ya watumishi wa zahananti yenye thamani ya shiilingi milioni 150.
Mh
kasesela aliwashukuru sana wadau wa maendeleo na kuwaomba kudumisha
ushirkiano na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa mkwawa Hunting
Safaris.