Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Maiko Lekule Laiser ,akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda, aliyepo kushoto kwa mkuu huyo ni mwenyekiti wa Taso kanda ya Kaskazini ndugu Athar Kitonga Shayo wakiwa katika uzinduzi wa maonyeho hayo ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Taso Themi nanenane Njiro Jijini Arusha. |
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda amewataka Wakurugenzi wote wa
Mikoa yote mitatu iliyopo Kanda ya Kaskazini ,wabadilishe mabanda yao na
wajenge ya kisasa zaidi kwaajili ya maonyesho ya wakulima na wafugaji
ambayo yatakuwa na mvuto zaidi.
Aliyasema
hayo alipokuwa kifungua maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika
viwanja vyaThemi nanenane Njiro Jijini Arusha,huku akiwataka Taso
washirikiane na Jiji pamoja na viongozi wa mikoa yote ili waweze
kutengeneza ukumbi mkubwa wa kisasa.
Aidha alisema kumekuwa na changamotoya wananchi.kutoielewa kauli mbiu
ya maonyesho ya nanenane mwaka huu hivyo basi amewaagiza wakulima na
wafugaji waweze kuingia.kwenye mafunzo ya shamba darasa na kwenye
mabanda ili waweze kupata elimu zaidi.
Aliwaagiza washiriki wenye mabanda yenye technolojia za
kilimo waandae taarifa fupi ambayo mwananchi atakwenda nayo nyumbani na
zitakazo waletea mabadiliko katika maeneo wanayotokea.
Sambamba na hayo aliwataka Taso kuangalia sheria viwanja vya
maonyesho ambayo inapiga marufuku ongezeko la makazi ndani ya viwanja
vya maonyesho,pia amewataka washiriki wote wa maonyesho watoe
ushirikiano kwa vyombo vyabulinzi na Usalama na katika maeneo yao.
Vijanana
wa JKT Oljoro wakiwa wanatoa burudani siku ya uzinduzi wa maonyesho ya
wakulima na wafugai ya nayandelea katika vianja vya Taso Themi nanenane
njiro Arusha.
Meya
wa Jiji la.Arusha wa pili kutoka kulia ndugu Calist Lazaro akiwa
wakiteta jambo na diwani wa kata ya Themi Melance .E.Kinabo wa kwanza
kulia katika maonyesho yanayoendelea katika maonysho yanayoendelea
katika viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo akiwa anatoa utambulisho.kwa.viongozi
mbalimbali waliohudhuria sikubyaufunguzi wa.maonusho ya wakulima na
wafugaji yanayondelea katika viwanja vya Themi Njiro.