Na Woinde Shizza,Arusha
Wakazi
wa Jiji la.Arusha na vuiunga vyake pamoja na kutoka mikoa jirani
wamefurika katika Tamasha linaloitwa LETS PRAISE SUMMIT, lililoandaliwa
na Mchungaji Adamu Haji katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano (AICC)
katika ukumbi wa Simba.
Maelfu ya watu hao walianza
kumiminika katika Kituo hicho cha Mikutano kuanzia saa tatu asubuhi
ambapo hata kabla tamasha hilo halijaanza tayari Ukumbi wa Simba uliopo
AICC ulikuwa umejaa na hivyo kusababisha maelfu ya watu waliofika
kuzuiliwa nje kwa kuwa kulikuwa hakuna namna ya wao kuingia ukumbini
kutokana na kufurika kwa watu.
Akielezea hali hiyo ya
maelfu ya wahudhuriaji wa tamasha kushindwa kuingia ukumbini, Muandaaji
wa tamasha hilo mchungaji Adamu Haji amesema kuwa hakutegemea kuwa watu
wangelikuwa na muitikio mkubwa namna hiyo hivyo amesema kuwa atamuomba
muimbaji huyo asiondoke mapema ili lirudiwe upya maana watu wwengi
wanatamani kumuona.
Mchungaji
huyo amesemakuwa wameamua kufanya tamasha hilo ndani ya ukumbi
kwasababu ya kutii agizo la serikali na wao hawataki kupingana na
serikali hivyo watajitahidi kulifanya tamasha hilo kwa mara ya pili ili
watu wote waweze kufaidi .
Kwa
upande wake Afisa Itifaki na uhusiano wa Aicc Rodney Thadeus amesema
kuwa ukumbi huo unauwezo wa kuchukua watu 1350 hivyo usingeliweza
kuhimili idadi kubwa ya watu ambao walitaka kuingia ukumbini hapo
kwaajili ya tamasha hilo.
Martha Uhwelo Muimbaji wa nyimbo.za.injili ambaye hakufanikiwa kuingia ukumbini.
Daniel Philipo Muimbaji.wa Nyimbo za injili ambaye na yeye hakufanikiwa kuingia.ukumbini katika tamasha hilo.
Kwa
upande waimbaji ambao hawakufanikiwa kuingia ukumbini kwenye tamasha
hilo wamesema kuwa waandaaji wa tamasha hilo hawajajipanga."Huwezi
kumleta muimbaji mkubwa kutoka kundi.kubwa linalifahamika.duniani la
Joyous Celebration kutoka Afrika ya Kusini ,kisha tamasha lifanyike
ukumbini"
"Kila
mtu amekuja hapa kwaajili ya kumunaona muimbaji Mkhululi Bhebhe,sasa
ona tunaondoka hata ukumbini hatujaingia kwasababu ya ukumbi mdogo siku
nyingine hawa waandaaji wakiandaa tamasha kama hili waliweke kwenye
uwanja kila mtu afaidi alisisitiza mmoja wa aliyekuja kwaajili ya
tamasha "
Muonekano wa ukumbi wa Simba ulivyofurika watu ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
Muimbaji
Daniel Safari akiwa anaimba katika Tamasha hilo katika ukumbi wa Simba
ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
Watu wakiwa nje ya Geti kuu AICC ambao wameshinndwa kuingia ndani ya ukumbi.
Muonekanonwa
watu mbalimbali kila mtu akijadili na mwenzake baada ya kuambiwa
hawawezi kuingia ndani ya ukumbi kutokana na ukumbi huo kufurika hivyo
wanalazimika kurudi majumbani mwao.
Sambamba
na hayo kiongozi wa kundi la Worshipers Aberdnego Hango ambao ni
wenyeji wa Muimbaji Mkhululi Bhebhe kutoka kundi la Joyous Celebration
kutoka Afrika ya Kusini amesema kuwa tamasha hilo ni kubwa mno watu
wamekuwa na muitikio mkubwa sana japo kuwa ukumbi umekuwa
mdogo,amewataka wale ambao hawajafanikiwa kuingia ukumbini wasivunjike
Moyo kwani season II inakuja hivi karibuni.