WATANZANIA WATAKIWA KUTHAMINI BIDHAA ZA NDANI





Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Old East International Moses Mwano akiwa anazungumza na wateja waliotembelea banda hilo katika Maonyesho yanayoendelea katika Viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Old East International Vivian Stephano akiwa anachukua kumbukumbu ya mteja Katika maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Taso Njiro Jijini Arusha.
Meneja mauzo wa Kampuni  Old East International akiwa anamfafanulia mteja juu ya Crown Cartridge,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane.
Afisa Mipango wa Kampuni Old East International Ephrahim Moses   Mwano akiwa anaonyesha Aina ya Wino wa Crown ambao wanatengeneza hapa nchini,Katika maonyesho ya wakulima na wafugaji Katika viwanja vya nanenane Njiro Jijini Arusha.
Na Woinde Shizza,Arusha
Wito umetolewa kwa Watanzania  watumie na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na kupatikana ndani ya nchi badala ya kuzipa kipaumbele bidhaa za nje ya  nchi.

Hayo yamesemwa  leo na Mkurugenzi wa Old East International ndugu Moses Mwano ,katika maonyesho yanayoendelea katika viwanja vya Taso nanenane  njiro Jijini Arusha.

Mwao amesema kuwa Watanzania wengi wanathamini bidhaa zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi,ambazo baadhi hazina kiwango cha ubora unaotakiwa kwa mtumiaji.

Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya  Old  East International amesema kuwa kampuni hiyo ni ya Kitanzania ,imesajiliwa na ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania wao ni wawekezaji wa ndani,wanahusika kutengeneza wino wa kuchapia unaofahamika kwa jina la Crown Cartridge.

Kwa upande wake Mwano amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli,katika jitihada zake za kuifanya Nchi kuwa ya Viwanda.

Sambamba na hayo amewaasa Watanzania watengeneze na kuingiza Bidhaa zenye kukidhi  ubora na viwango ,huku akimalizia na msemo usemao " kizuri cha jiuza kibaya chajitembeza akimaanisha kuwa ukitengeneza bidhaa nzuri yenye kukidhi viwango na ubora unaohitajika wateja watafurahiwa nayo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post