Taarifa mpya kwa wadau wa mitindo na fashion + vyombo vya habari inasema hivi, Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin kutoka Tanzania anategemea kuiwakilisha Tanzania kwa kuonesha mitindo yake katika jukwaa kubwa la biashara nchini Marekani katika mji mkuu wa California, Sacramento.
Show hiyo inatambulika kama 'The African Trader Show', Tamasha litafanyika siku 3 kuanzia Tarehe 2 mwezi wa 9/2016 - 4/9/2016. Mbali na Asya pia Mr. Yasin Kapuya atawakilisha Tanzania kwa kutoa mada na kuonesha ufundi wa kazi zake katika onesho hilo. Hivyo ndugu jamaa na marafiki + Watanzania kwa ujumla tunapaswa kutoa ushirikiano wadhati kwa Wanzanzania hao.