kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
Mchimbaji
wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa
Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani
Akithibitisha
kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani
baada ya kutumia moto wa mkaa
Alisema marehemu huyo aliwasha moto wa mkaa kulainisha mwamba ili aweze kupata maji
Pia alisema kisima hicho akichokuwa anachimba chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha
"Kilichotokea
ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa
ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika , "alisema
"Mwili wa marehemu haujakutwa na jera lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda.
Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha..