Na Sheila Simba- MAELEZO
Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William
Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya kupima ardhi nchi nzima kuanzia mkoani Morogoro.
Akizungumza katika
kipindi kipya cha "TUNATEKELEZA" kinachoandaliwa na Idara ya
Habari-MAELEZO na TBC1 ,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo
ili kupima maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani
humo.
“Serikali tumedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi,
kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na migogoro ya ardhi isiyo na
tija inayosababisha watu kupoteza maisha’’Alisema Lukuvi
Ameongeza kuwa
katika upimaji huo wa ardhi serikali inashirikiana na kampuni binafsi
zilizosajiliwa ili kumuwezesha mwananchi anayemiliki shamba,kiwanda ,mkulima na
mfugaji mwenye eneo kupimiwa na
kuongezewa thamani.
“Nakuhakikishia
katika kipindi cha miaka 10 kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa kimepangwa
na kupimwa utaratibu mzuri utakao mwezesha kila mtumiaji wa ardhi kutumia eneo
lake”alifafanua Lukuvi.
Pia ameeleza suala la kuthibiti bei ya kupima ardhi kwa
kushirikiana na wapimaji binafsi katika kumfanya kila mtanzania alipe bei
halali ya kupima ardhi.
Aidha amesme kuwa Serikali itaweka ukomo wa kumiliki
ardhi ili kuondoa tabia za watu kumiliki eneo kubwa la ardhi bila ya
kuliemdeleza kwa muda mrefu.
“serikali itaweka muda wa mtu kumiliki ardhi, haiwezekani
mtu mmoja amiliki eneo hata bila kulitumia, tabia hii itafika mwisho.”
Akizungumzia suala la wageni kumiliki ardhi alisema kuwa
ni marufuku kwa wageni na wawekezaji kununua ardhi vijijini bila kupitia wizara
inayohusika.
“Ni marufuku kwa mgeni au mwekezaji kwenda kijijini
kununua ardhi bila kuja kwangu au Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),wakifanya
hivyo tutawapa ardhi wawekeze, Pia mtu yeyote anayetaka kujenga kiwanda popote
afike ofisini kwangu nitampatia ardhi ndani ya siku saba.”alisema Lukuvi
Ameongeza kuwa
Wizara imetenga viwanja 240 kwa ajili ya Viwanda enoa la Kigamboni ili
kutimiz lengo la Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Mbali na hayo Waziri Lukuvi alisema wananchi wote waliodhulumiwa viwanja Jijini
Dar es Salaam kwa makosa ya watendaji wa Serikali wameanza kupewa viwanja vingine mbadala.
“Naagiza Halmashauri zote ziwapatie viwanja mbadala
wananchi ambao walidhulimiwa viwanja vyao kwa makosa ya watendaji.”