Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Arusha
aliyetambulika kwa jina la Victoria Wenga (51) mkazi wa Lemara jijini Arusha
amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia jana kwa kutumia shuka lake bila
ya Mount Meru.
kuacha ujumbe wowote.
Marehemu alikamatwa Agosti 21 mwaka huu majira ya Alfajiri kwa tuhuma za
kuchoma moto nyumba yake na maduka yake mawili kutokana na ugomvi wa
kifamilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kutokea kwa tukio
hilo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi saa 6:20 usiku jana wakati wenzake
wakiwa wamelala.
“Polisi wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike
ambapo polisi walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini
ilishindikanika,” alisema Kamanda Mkumbo.
Mahabusu huyo, ambaye ni mkazi wa Lemara jijini Arusha, alijinyonga kwa
kutumia shuka lake alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko mahabusi.
Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka
yake.
“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa linamkabili,” alisema
Kamanda Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya usalama kituoni hapo na
tukio hilo, havihusiani na sababu zozote za kiusalama.
Marehemu Victoria anadaiwa kuwa na ugomvi wa kifamilia na mume wake
aliyetambulika kwa jina la Edward Wenga akimtuhumu kuzaa nje ya ndoa
kinyume na utaratibu.
Imeelezwa kuwa hicho ndo chanzo cha marehemu kufikia hatua ya kuteketeza
mali walizochuma na mume wake ambazo ni maduka mawili na nyumba ya
kuishi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali
ya Mount Meru.