UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIKE NA MFUMO MZIMA WA MAPENZI ( SEX) KWA MWANAMKE

 SEHEMU YA 1: UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIKE NA MFUMO MZIMA WA MAPENZI ( SEX) KWA MWANAMKE



NUKUU: “katika kila wanawake 8,mwanamke mmoja ana matatizo ya nguvu za kike”

.

Bila shaka sote tunafahamu furaha na faida za kufanya mapenzi kwa mwanamke na mwanamke. Kama ambavyo mwanaume hufurahia tendo la ndoa kwa kufika mshindo basi mwanamke nae pia hufurahia kwa kufikia mshindo. 

.

Wanaume wengi wamekua wanafurahia tu wenyewe bila kujali kama mwanamke kafurahi au la jambo ambalo si zuri kabisa.

.

 Kadhalika wanawake wengi hawana uzoefu na kitu kinachoitwa mshindo au kwa lugha ya mtaani kukojoa na hivo kuwawia ugumu kuelewa kama wana tatizo hilo au la. 

.

Kutokana na kuongezeka kwa utoaji wa elimu wanawake wengi wameanza kujitambua na kuanza kufuatilia afya zao kwenye suala ya kuridhika kimapenzi.

.

 Kutokana na sababu mbalimbali matatizo haya yanaweza kuanza kipindi mwanamke ndo anaanza mapenzi na kuendelea au akawa amepata tatizo hilo baada ya muda fulani.

.

Katika suala la upungufu wa nguvu za kike na matibabu yake hutegemeana sana na kisababishi,ukubwa wa tatizo ,utayari wa mlengwa na kama kisababishi kinajulikana au la
.
Upungufu wa nguvu za kike ni ile hali ambayo mwanamke hafurahii tendo la ndoa na kwa kutokufurahia kunamletea msongo wa mawazo,mdororo wa amani ,mdororo wa mahusiano pamoja na mdororo wa afya kwa ujumla.  

Hali hii inaweza kuja katika sura zifuatazo:
.
1️⃣Kushindwa kufika mshindo ama kukojoa (inability to achieve orgasm)

2️⃣kushindwa au msisimko mdogo wakati wa mapenzi (impaired arousal)

3️⃣ wakati wa tendo la ndoa (pain with sexual activity)

4️⃣Kukosa hamu ya mapenzi au hamu ya mapenzi kupungua (lack of sexual desire)

MFUMO WA MAPENZI ULIVO KWA MWANAMKE

itaendeleaaaa….

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post