Mtaalamu wa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu Kwa tiba asili ambaye pia ni Mkurugenzi wa kazoba international herbal products Dkt Mwasiga Kazoba akitoa maelekezo Kwa wateja wake ambao ni wagonjwa waliofika ofisini kwake zilizopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha namna dawa zake za asili zinavyofanya kazi
Na Woinde Shizza,Arusha
Katika ulimwengu wa leo unaohitaji nguvu katika kazi na biashara, baadhi ya watanzania wamebainika kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara na kusahau kuwa Kupima afya kunaweza kuokoa maisha na kuzuia matatizo yanayoweza kuepukika.
Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu kwa tiba asili ambaye pia ni Mkurugenzi wa kazoba international herbal products Dkt Mwasiga Kazoba wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kutokujua hali yao ya afya jambo ambalo linaweza kuwa kuwa hatari kwao.
Alisema kuwa anapenda kuwahimiza watanzania kuweka umuhimu sawa kati ya majukumu yao ya kila siku na kutunza afya zao kwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kwani ni njia nzuri ya kutambua mapema matatizo yanayoweza kujitokeza na kuchukua hatua mapema.
‘’Kubadilisha mtazamo wetu kuhusu afya ni muhimu,afya siyo tu kujisikia vizuri leo, bali ni uwekezaji wa maisha marefu na yenye furaha ,tushirikiane katika kuhamasisha wenzetu, marafiki, na familia kufanya uchunguzi wa afya,ili tuweze kujenga jamii yenye nguvu na afya bora’’alisema Dkt Kizoba
Alisema kuwa ni wakati wa kila mmoja wetu kumuhamasisha mwenzake kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa afya na swala hili kuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku
‘’Tuanze kufanya maamuzi mazuri kwa afya zetu, tukitambua kuwa afya yetu ni mali Kwa kufanya hivyo, tutajenga jamii yenye uelewa wa kina wa umuhimu wa kupima afya mara kwa mara”alibainisha Dkt Kizoba
Aidha alimtaka kila mtanzania kumuhimiza mwenzake kufanya mazoea ya kupima afya, kwa kushirikiana na taasisi za afya kutoa elimu, na kuondoa vizuizi vinavyoweza kuzuia watu kufanya uchunguzi,huku akisisitiza kuwa Kupima afya isiwe ni jambo la dharura tu, bali iwe ni mtindo wa Maisha kwa kila mt una kwa pamoja, wafanye swala la kuchunguza afya kuwa sehemu ya utamaduni wao wa kila siku kwani wakiimarisha jamii yenye afya, furaha, na maendeleo.
Aliongeza kuwa Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa afya zao ndio mitaji yao mikubwa hivyo wametakiwa kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ya miili yao ili kuepuka matatizo makubwa ya kiafya huku akisisitiza kauli mbiu yao ya kizoba kuzingatiwa inayosema ‘afya yako ndio mtaji wako wa kwanza.