Na Woinde Shizza , ARUSHA
Wito umetolewa Kwa wazazi wote wanaopeleka watoto wao katika vyuo mbalimbali ,kuchunguza vyuo hivyo kwanza kama vimesajiliwa kwani kumekuwepo na changamoto ya uwepo wa vyuo vingi vinavyotoa elimu bila ya kuwa na usajili wa serikali
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa vyuo vya ufundi Kanda ya kaskazini (VETA)Monica Mbelle wakati akiongea katika mahafali ya nane ya chuo cha Volcano yaliyofanyika leo chuoni apo ambapo alibainisha kuwa kumekuwepo na tatizo la wazazi kupeleka watoto katika vyuo mbalimbali bila ya kuangalia vyuo hivyo vimesajiliwa na serikali au la .
Amebainisha kuwa madhara ya kupeleka mtoto katika vyuo ambavyo avijasajiliwa ni pamoja na kushidwa kupata kazi katika taasisi mbalimbali ikiwemo za serikali huku akifafanua kuwa Kwa kipindi hichi serikali imekuwa ikitangaza na kutoa kazi kupitia mfumo hivyo iwapo mwanafunzi ataomba kazi na alisoma katika chuo ambacho avijasajiliwa basi mfumo hauta mkubali na atakuwa amepoteza rasilimali muda ,fedha na umri kusoma sehemu ambayo haitambuliki
Aidha alimshukuru na kupongeza Rais wa Samia Kwa kuanziasha vyuo vya ufundi stadi Kila wilaya kwani vinasaidia wananchi kupata huduma Kwa urahisi,huku akiwataka wazazi Kutumia vyuo hivyo kuwapeleka Watoto wao kupata elimu ya ufundi stadi ambao kwa Sasa ndio sehemu kubwa ya ajira ndio zinapatika huko
Kwa upande wake mkuu wa chuo Cha Volcano Lazaro Thobias alisema kuwa haya ni mahafali ya nane na jumla ya wanafunzi 87 wamehitimu katika kozi mbalimbali ikiwemo ya utalii,ufundi umeme wa tanesco na magari ,hotelia ,urembo pamoja na lugha mbalimbali ambapo alibainisha
kuwa chuo Chao kinatoa kozi za muda mrefu na mfupi
Aliwataka wanafunzi waliosoma kozi fupi kutobweteka na kuona wamemaliza bali wajitaidi kuongeza elimu zaidi kwani Kadri siku zinavyozidi kwenda ndio mambo mapya yanavyozidi kuongezeka
.