MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Freeman Mbowe anatoa maagizo kwa viongozi wapya wa chama hicho kuunda tume kwa ajili kuyaponya majeraha yaliyotokana na kampeni za uchaguzi uliomuondoa madarakani.
Mbowe ameyasema hayo leo tarehe 22 Januari 2025 alipokuwa akiwaaga wajumbe na wanachama wa chama hicho mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Chama katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
"Kwa namna wagombea mbalimbali walifanya kampeni zao zimeacha majeraha mengi, tusipolitibu jambo hili litaharibu brand ya chama chetu".
"Mimi niliahahidi nikishinda nitaunda tume ya kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi, nazungumza kama Baba wa Chama hiki, nawaagiza katibuni majeraha haya undeni tume haraka ya kuponya majeraha" Ameeleza Mbowe.
Aidha amewahasa viongozi hao kutokufanya jambo jambo kinyume cha Katiba ya chama hicho.
Tags
HABARI MATUKIO