Siku ya Shukrani kwa Mlipakodi: Rais Samia Kuonyesha Mshikamano na Walipakodi Bora

 

Jumla ya Walipakodi 1228 kutoka kona zote za Tanzania, wanatarajia kukabidhiwa zawadi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan katika Siku ya shukrani kwa Mlipakodi itakayofanyika January 23, mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22.01.2025 Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo amesema zawadi hizo zitatolewa kwa Walipakodi waliyofanya vizuri katika kulipa Kodi kwa kipindi cha Julai 2023 mpaka June 2024.

Kayombo ametaja vigezo walivyotumia kuwachagua wanaopewa zawadi ikiwemo Mlipakodi kodi mwenye rekodi nzuri katika ulipaji wa Kodi, Mlipakodi kwa hiari na kwa wakati, Mlipakodi anayetumia EFD mashine kikamilifu, Mlipakodi aliyelipa kodi kubwa zaidi na Mlipakodi anayetoa ushirikiano kwa TRA.

Kayombo amesema zawadi hizo zitachagiza Walipakodi wengine kufanya vizuri zaidi ili na wao watunukiwe wakati ujao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post