BOLT YAZUA GUMZO ARUSHA AJIRA ZA VIJANA NA WANAWAKE ZAPAA



Na Woinde Shizza ,Arusha

 Mkutano wa wataalamu wa mawasiliano zaidi ya 100 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umefanyika jijini Arusha na kuibua mijadala mikubwa kuhusu uaminifu kati ya wananchi na taasisi pamoja na nafasi ya sekta binafsi katika kuboresha huduma.

Mkutano huo unaojulikana kama East Africa PR Week umehusisha maofisa uhusiano kutoka sekta mbalimbali huku kampuni ya usafiri wa mtandaoni Bolt ikivuta hisia za wengi kutokana na mchango wake katika kuleta ajira na kuchochea uchumi wa Tanzania.



Akizungumza kwenye mkutano huo 

Meneja mahusiano ya umma kampani ya kimataifa ya usafiri bolt Tanzania Gilbert Ginono

 imekuwa sehemu muhimu ya mabadiliko ya kiuchumi nchini na imewafungulia vijana wengi milango na kutoa fursa za kujipatia kipato  kupitia shughuli za uendeshaji na usafiri wa mtandaoni.

 Amesema vijana wengi sasa wanategemea Bolt kupata kipato cha kila siku na kwamba mfumo huo wa kidigitali umeongeza mzunguko wa fedha na kutoa matumaini kwa wanaotafuta ajira mijini.

Ginono amesema pia kuwa Bolt imekuwa msaada mkubwa kwa wanawake wanaotaka kuingia kwenye sekta ya usafiri ambapo idadi yao imeongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni. 

Ameeleza kuwa uwepo wa wanawake kwenye mfumo wa Bolt umeongeza usawa wa kiuchumi na kutoa nafasi kwa familia nyingi kuinuka kimaendeleo.

Aidha amesema huduma ya Bolt imeongeza ushindani katika sekta ya usafiri wa mijini na kuleta ubora wa huduma pamoja na fursa mpya za kifedha kwa madereva katika mikoa mbalimbali ya nchi huku  akisisitiza kwa kusema  Bolt haijaja kutoa huduma pekee bali imekuja kujenga ajira endelevu na kuchangia pato la taifa kupitia teknolojia.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Chama cha Maofisa Uhusiano Tanzania Bwana Loti Makuza alisema mkutano huo umelenga kuongeza uelewa kwa maofisa uhusiano ili wawe tayari kuijenga imani kati ya serikali na wananchi.



 Alisema maofisa uhusiano wanatakiwa kuifahamu taasisi yao kwa undani ili waweze kutoa ufafanuzi sahihi wanapoulizwa na umma.

Makuza alisema haiwezekani afisa habari kuulizwa swali kuhusu taasisi yake halafu akose majibu kwa kisingizio cha kwenda kuuliza viongozi wake kwa sababu jambo hilo linashusha taswira ya kitaaluma.

 Amefafanua kuwa maofisa uhusiano wa sekta binafsi wanaonekana kufanya vizuri zaidi kutokana na kushiriki vikao vya maamuzi na kujua undani wa taasisi zao tofauti na wenzao wa sekta ya umma.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia