Mgeni
Rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Mh. Philipo Mulugo akihutubia wahitimu na
wageni waalikwa kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo cha Ufundi Arusha
(ATC).
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha, Bw. Abraham Nyanda akitoa
Hotuba wakati wa Mahafali.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi, Eng. Dkt. Richard Masika akitoa Hotuba wakati
wa Mahafali ya Tano ya Chuo.
Wafunzi
bora Kumi (10) wakiwa wameshikilia Mfano wa Hundi ya Sh. Mil 10 wakiwa
katika picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Mh. Philipo Mulugo pamoja na baadhi ya Wageni Waalikwa. Fedha
hizi ni Ahadi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Mizengo Peter Pinda (MB) kwenye mahali ya Nne na Tano.
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
kimedhamiria kutumia wanafunzi pamoja na wakufunzi wao kubuni teknolojia
rahisi itakayoweza kumaliza tatizo la umeme maeneo ya vijijini.
Kwa mfano, Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
kimedhamiria kutumia wanafunzi pamoja na wakufunzi wao kubuni teknolojia
rahisi itakayoweza kumaliza tatizo la umeme maeneo ya vijijini.
Mhandisi Urbanus Melkior, ni Mkuu wa Idara ya
Umeme chuoni hapo, anayeamini kuwa wanafunzi wao kwa kushirikiana na
wakufunzi, wanaweza kusaidia kutatua tatizo la umeme vijijini.
Katika kutekeleza hilo, anasema chuo hicho
kimebuni mtambo mdogo wa kufua umeme ujulikanao kwa Kiingereza ‘Mini
hydro Turbines’, unaotumia maji kwa kiasi kidogo.
“Mwaka 2011 kulikuwa na mgao mkubwa wa umeme. Watu
walikuwa wanakaa bila umeme kwa kati ya saa nane mpaka 11, hali hiyo
ilitufanya tufikiri jinsi tutakavyoweza kufanya, ili kupata ufumbuzi wa
tatizo la umeme,” anasema.
Anaeleza kuwa, baada ya hapo idara ya umeme
ilishirikiana na idara ya mitambo hatimaye walifanikiwa kutengeza mtambo
huo ambao umefungwa katika eneo la Makumira wilayani Arumeru.
Melkior anasema kwamba, mtambo huo unaweza
kuzalisha umeme kwa kutumia maji kidogo yanayopita kwenye mfereji. Kwa
sasa takriban kaya 20 zinahudumiwa na umeme huo.
“Tunachofanya sisi ni kutengeneza mtambo na kwenda kuufunga, tukimaliza tunawaachia wanakijiji wanaoutunza,” anasema.
Anaeleza kuwa, teknolojia iliyotumika kuutengeza
ni rahisi na inaruhusu mtu yeyote hata asiyekuwa mtaalamu wa umeme
kuweza kuuhudumia mtambo huo.
“Mtambo ukishawekwa, kazi itakayokuwa inafanyika
ni kufungulia maji yaje kwenye mtambo ama kuyapunguza, nyingine ni
kupaka vilainishi tu, hii anaweza kufanya mtu yeyote,” anaeleza.
Mbali ya Makumira, mtambo huo pia umefungwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Morogoro, Iringa , Katavi, Njombe na Ruvuma.