Watumiaji wa gesi kwenye mitungi mikubwa na midogo hapa nchini
wanaibiwa gesi hiyo kwa sababu wananunua bidhaa hiyo bila kupimiwa ujazo
kwenye mtungi.
Bi. Irene John ambaye ni Kaimu Msemaji wa
Wakala wa Vipimo Nchini alisema mtungi wa gesi una uzito wa kilo 15 na
gesi yenyewe lazima iwe na ujazo wa kilo 15 jumla mtungi unatakiwa kuwa
na kilo 30, lakini wakazi wengi wanauziwa hizo gesi bila ya kupimiwa na
hivyo kuchukua mitungi ambayo haijatimia na baada ya wiki unakuwa
imekwisha.
Kwa upande mwingine, katika kukagua na kupima mita za Luku kujua kama
kweli mita inanyonya umeme kawaida au wanawaibia Tanesco au anaibiwa
mwananchi, kwa sasa wana changamoto kubwa ya kuwa na vipimo vya kupima
mita za luku ili kujua unyonyaji wa umeme, vikipatikana vipimo vya
kupima mita za luku basi malalamiko kwa wananchi yatapungua.
Nchi zote duniani lazima kuwe na maabara ya kupima umeme, gesi,
vyakula, mafuta na vitu mbalimbali, vipimo hivyo lazima vinasibishwe kwa
ubora wa hali ya juu kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Vyuo vingi kwa sasa hawakuingiza mitaala ya vipimo kwa sasa chuo
kimoja tu nchi mzima nacho ni CBE, kwa sababu hiyo wataalumu wa upimaji
hapa nchini ni wachache kutokana na kuwa kuwa na chuo kimoja tu cha
kutoa taaluma hiyo ya upimaji.
Kufuatia hali hiyo ya kuwa na wataalamu wachache katika suala la
vipimo wataendelea kuwaelimisha wakuu wa vyuo mbalimbali hapa nchini ili
kuweza kuanzisha mitaala ya upimaji na kuwa na wapimaji wengi.
Sheria ya mtu akizidisha mazao kama kwenye magunia kwa kujaza rumbesa
inamlinda sana mfanyabiashara na kumkandamiza mkulima, sheria hiyo ya
mwaka 1982 inasema kuwa mfanyabiashara akijaza rumbesa anapiga faini ya
10,000 au jela mwezi mmoja, sheria hiyo inachangia wafanyabiashara
waendelee kupeta.
Leo ni siku ya Kimataifa ya Vipimo Duniani kauli mbiu ya mwaka huu Vipimo na Changamoto ya Nishati Duniani.