WAASI WA SELEKA WAENDELEA KUJIIMBARISHA ZAIDI

selekaKundi la waasi la Seleka (pichani) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limesema limejipanga upya ili kuendelea kuwashikilia vizuri wapiganaji wake.

Serikali imelaani hatua hiyo, na kusema kundi hilo limeshikilia mali za nchi kaskazini mwa nchi hiyo.
Kundi hilo la waasi Waislamu limekuwa likihusika na mapingano na wapiganaji wa Kikristo wa wanamgambo wa anti-balaka tangu mwezi Machi 2013.
Vita hivyo vimesababisha asilimia 25 ya watu kupoteza makazi yao kati ya idadi ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati milioni 4.6.
Umoja wa Afrika, Ufaransa na Umoja wa Ulaya wana vikosi vipatavyo 7000 vinayopambana kumaliza vita hivyo nchini humo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post