Askofu Sixbert Paul wa kanisa la Victorious la mjini Moshi akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na hafla ya kutunukiwa shahada la udaktari ya huduma |
Askofu Sixbert Paul wa kanisa la Victorious la mjini Moshi akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na hafla ya kutunukiwa shahada la udaktari ya huduma |
CHUO kikuu cha Africa, African Graduate University, Chenye makao yake nchini, Sierra Leone kinatarajia kumtunuku shahada ya udaktari ya huduma, Askofu Mkuu Sixbert Paul, wa kanisa la Victorious, lenye makao yake makuu mjini Moshi, mkoani Kilimajaro, katika hafla itakayofanyika Jumapili hii.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Askofu Sixbert alisema atakabidhiwa shahada hiyo jumapili ya May 18 mwaka huu katika kanisa la Victorious lililopo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Askofu Sixbert alisema pamoja na yeye kutunukiwa shahada hiyo, pia mwimbaji wa nyimbo za injili Rose Mhando,atatunukiwa cheti maalumu cha kutambua mchango wake wa kueneza injili kupitia uimbaji.
Alisema katika hafla hiyo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Meya wa Mji wa Mshi Bw. Jafary Michael, na kwamba viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika Kusini, Zambia,Uganda , Kenya na Kongo watahudhuria, akiwemo mpatanishi wa masuala ya kijeshi anayefanya kazi na umoja wa mataifa Brigedia Timoth Kazembe ambaye anatoka nchini Zambia.