Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal
JituSon mara baada ya kuwasili na kupokelewa katika Kata ya Mangara
wilaya ya Babati Vijijini.Katibu Mkuu wa CCM yupo ziarani katika mkoa wa
Manyara ambapo atafanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kukagua
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukagua uhai wa
chama.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amezungukwa na wakazi wa
Kata ya Mangara wilayani Babati Vijijini waliojitokeza kwa wingi
kuwapokea mara baada ya kuwasili wilayani hapo .
Wananchi
wa Kata ya Mangara wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mapokezi ya
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya
Mangara kabla ya kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya kituo cha afya cha
Mama na Mtoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal
JituSon mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya kituo cha afya
cha mama na mtoto.Katibu Mkuu wa CCM yupo ziarani katika mkoa wa
Manyara ambapo atafanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kukagua
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukagua uhai wa
chama.
Wananchi wa Kijiji cha Mangara wakionyesh bango la kuomba msaada wa kusaidiwa kujengwa kwa daraja katika mto Mangara.
Mto Mangara ambao wananchi wanaomba daraja lijengwe.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Magugu ambapo
aliwapa usia vijana wenzake kwa kuwaambia Vijana wachape kazi na
waachane na talalila za wanasiasa njaa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Magugu na
kuwaambia viongozi wengi wa vijiji wamekuwa wakiingia mikataba bila
kuwashirikisha wannchi hivyo kusababisha migogoro mikubwa ya ardhi na
amewataka wananchi kuchagua viongozi makini,Katibu Mkuu wa CCM
ameshtushwa na baadhi ya watu kumiliki sehemu kubwa ya ardhi na
kuwakodishia wananchi kwa ajili ya kilimo cha mpunga.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia