TAMASHA LA MTU KWAO LAANZA KUTIMUA VUMBI ARUSHA ,NGOMA MBALIMBALI ZARINDIMA

 mmoja wa wawadau wa utamaduni akiwa anawaonyesha malagwanani jinsi ya kutumia mishale
 wanafunzi wakiwa wanapewa mafunzo ya kutengeneza magari ya mabati
 machifu wakibadilishana uzoefu na ukabila wao
 malagwanani wa kimasai wakiwa katika picha ya pamoja



 chifu wa  kinadi  ambayo ipo katika wilaya ya Itilima  mkoani Simuyu  Wenceslaus Clement  akiwa anabadilishana mawazo na malagwanani wa kimasai
 mkutunzi wa kabila la wabarabaigi akiwa anawaonyesha malegwanani wa kimasai mishale ya sumu ambapo alisema kuwa mishale hiyo ina sumu kali ambayo imetengenezwa na miti aina saba ambayo ikikupiga tu auwezi kukimbia ata hatua ishirini kabla ujaanguka na dawa yake aipatikani hospitalini zaidi ya wao wenyewe wanaotengeneza mishale hiyo kukupa dawa

 maandalizi ya machalari yakiendelea
 chifu   Gilbert Rugal Isambe akiwa anapokea maelezo ya jinsi ya kutengeneza nguo za kabila ya kibarabaigi  kutoka kwa mkufunzi wa kabila hilo ambalo jina atukuweza kulipata
 mnyama aina ya ngamia nae pia aliletwa kwa ajili ya kuwa kivutio katika tamasha hili na hapa wananchi na wanafunzi wakiwa wanawaaangalia wanyama hao
 mwanadada wa libeneke la kaskazini akiwa amejumuika na waimbaji wa ngoma ya kichaga wakiwa wanacheza pamoja hii yote ni kuuenzi utamaduni wetu
 wanafunzi wa shule za msingi nao walikuwepo wanaendelea kuburudika na ngoma
 vyakula vya jadi vikiwa vinaendelea kupikwa live

 picha ya juu na chini ni maandamano ya machifu kutoka mikoa mbalimbali yakiwa yanaingia katika uwanja wa sheikh Amri Abeid kwa ajili ya sherehe za tamasha la  MTU KWAO lililoanza kufanyika jijini hapa
waandishi wa habari akiwemo mdada mdada wa woindeshizza blog wakiwa wanaburudika na chakula cha jadi ya kimasai kiitwacho loshoro

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post