WACHEZAJI WATATU WA TANZANITE FC MBARONI KWA KUMSHUSHIA MUAMUZI KIPIGO CHA MBWA MWITU

Waamuzi na washabiki wakimuamua Refa aliyekua akipokea kipigo toka kwa wachezaji wa Tanzanite Fc

Kipa wa Tanzanite akiwa ameshikwa wakati akitaka kukimbia baada ya kumshushia kipigo Refa

 Mmoja wa watuhumiwa Akiwa katika mikono mikakamavu ya Polisi

Mwamuzi wa Mchezo akiyeshushiwa kipigo akipatiwa matibabu baada ya kuokolewa


Kiongozi wa Waamuzi ndugu Jumbe akitoa maelekezo kwa waamuzi baada ya mchezo kuharibika

Wamuzi wakishauriana Kabla ya kumaliza mchezo baada ya Timu ya Tanzanite kutorudi uwanjani


Kiongozi wa Waamizi ndugu Jumbe akiwatuliza waamuzi kuacha kujadili tukio lililotokea na kujiandaa na mchezo

Wachezaji wa AFC ya Arusha wakisali baada mchezo kuisha wakiwa wanaongoza kwa goli mbili bila dhidi ya Wachimba Madini Tanzanite Fc


MBEYA leo katika uwanja wa vwawa uliopo Wilaya ya mbozi jijini mbeya kunaendelea mashindano ya ligi daraja la pili katika ngazi ya mabingwa wa mkoa. Ligi hiyo ikiwa imefikia katika mzungukowa tano hivi leo ambao umewakutanisha Timu mbili kutoka kanda ya Kaskazini ambazo ni AFC kutoka jijini Arusha na timu ya Tanzanite Fc kutoka mkoani Manyara.

Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi mnamo saa nane kamili, Ukiongozwa na muamuzi ndugu Bitebo Manduta huku kila timu ikionesha hari ya kuibuka na ushindi ndipo hali ilipobadilika mnamo dakika ya 15 pale AFC ilipoandika Goli lake la kwanza.Mpaka dakika ya 38 kipindi chakwanza AFC ilipoongeza Goli lapili mpakakipindi chakwanza kilipokwisha matokeo bila kubadilika.

Katika Kipindi cha pili kilipoanza Timu ya Tanzanite ilionesha mashambulizi huku kukiwa na uwalakini kila walipofika katika lango la Timu pinzani walionekana kusuasua kufunga kitendo kilichohamsha hisia tofauti kwa mashabiki huku wakipiga kelele kuwa wameuza mechi. Kelele hizo zilizua taharuki nakusababisha mashambulizi yaliyozua makosa ya mchezaji wa Tanzanite ndipo refa alipompa adhabu ya kadi ya njano kitendo ambacho kilisababisha Wachezaji wa Tanzanite kumzonga refa huku wakitoa maneno ya kejeli. Jitihada ya Refa kuwatuliza ziligonga mwamba ndipo alipoongeza adhabu kwa mchezaji na kumpa kadi nyekundu kitendo kilichoashiria kuwa walikua wakisubiria kadi hiyo ndipo walipoanza kumshushia kipigo Refa huyo. Na kuokolewa na Polisi wa kutuliza ghasia aliokua uwanjani hapo na kufanikiwa kuwakamata wachezaji watatu waliomshambulia Refa huyo.

Hata hivyo nilipata fursa ya kuzungumza na muamuzi aliyekua akitazama mpira katika benchi la mashabiki juu ya hatima ya timu ya Tanzanite na wachezaji waliotiwa nguvuni aliweza kubainisha kuwa kutokana na kanuni za michezo kwakosa hilo kuna uwezekano wa timu husika kunyang'anywa pointi zao na kufungiwa kabisa ila pia aligusia kidogo kuhusu wachezaji waliotiwa nguvuni kuhusika na shambulio hilo dhidi ya muamuzi alisema kwa kuwa muamuzi kaelekea polisi sasa hiyo ni kesi na ni kesi ya jinai ya kushambulia na kudhuru mwili hadharani na kesho weachezaji hao wana uwezekano wa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka hayo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post