Mwandishi wetu, Moshi
MFUKO wa
maendeleo wa wananchi wa Tarafa ya Kibosho wilaya ya Moshi
Vijijini,umetoa ahadi ya zawadi ya pesa taslimu shilingi Milioni moja
kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio la wizi
wa lami mali ya mfuko huo.
Ahadi
hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa mfuko huo, Morris Makoi katika
mkutano mkuu maalumu wa wanachama wa mfuko huo kufuatia wizi wa mapipa
35 uliofanywa na watu wasiojulikana Apili 17 mwaka huu.
Lami
hiyo ambayo imedumu kwa maiaka 17 sasa,imekuwa haina uangalizi mzuri
kutokana na kukosekana kwa ulinzi wa uhakika na kutoa mwanya kwa wezi
kuiba kiurahisi bila kukamatwa.
Akizungumza
katika mkutano huo ambao hata hivyo uliahirishwa kutokana na kutofia
idadi stahiki ya wajumbe,Makoi alisema kuwa,mtu yeyote mwenye taarifa
sahihi juu ya nani aliiba lami hiyo na wapi imeuzwa,awasiliane na
uongozi wa KIDEFU .
Mfuko
huo wa maendeleo ya wananchi wa tarafa ya Kibosho ulianzishwa kwa lengo
la kuharakisha maendeleo kwa wananchi ikiwamo ujenzi wa shule,hospital
na kuboresha miundombinu ya barabara .
Katika
kufanikisha mfuko huo,wananchi walikuwa wakikatwa shilingi mbili kwa
kila kilo moja ya kahawa kwa ajli ya kutunisha mfuko huo na lami hiyo
ilikuwa itumike kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Hata
hivyo mfuko huo uliyumba na kusambaratika na hivyo kushindwa kufikia
malengo yaliyokusudiwa ambako kwa sasa wananchi wameamua kwa makusudi
kuufufua mfuko huo.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti makoi ambaye pia ni diwani wa kata ya Okaoni na
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi,wizi huo unatokea kutokana
na kutokuwapo na usimamizi mzuri wa mali za mfuko huo kwa miaka kumi
sasa..