wauguzi wakiwa wanaingia uwanjani kwa maandamano
rais jakaya mrisho kikwete akiwa anasalimiana na baadhi ya wauguzi
wakati alipokuwa anatembelea mabanda katika maathimisho ya siku ya
wauguzi duniani ambapo kwa tanzania imefanyikia Arusha
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza kwa makini jinsi wauguzi
wanavyotoa huduma ya afya kwa wagonjwa wakati alipotembelea mojawapo ya
mabanda ya maonyesho ya Wauguzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi
Duniani yaliyofanyika kitaifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh
Amri Abeid mjini Arusha leo.
Wauguzi
wakiandamana wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani wakiwa na
mabango mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid Jijini
Arusha leo.
Wakimsikiliza Rais Jakaya wakati akihutubia.
Wauguzi
wakiandamana wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani wakiwa na
mabango mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid Jijini
Arusha leo.
Wito umetolewa kwa wananchi kujitaidi kupima afya zao kabla ya kutumia dawa,hayo yameelezwa leo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akihutubia katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Arusha
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kupima afya yake kabla ya kunywa dawa kwani itamsaidia kujua nini au ugonjwa gani unamsumbaua
Aidha Kikwete akiongeolea ugonjwa wa denguae alisema kuwa ugonjwa huu uliongia hapa nchi ni hatari hivyo ni wajibu wa kila mtanzani anahakikisha anauthibiti ugonjwa huu.
alisema kuwa iwapo kila mtu atafuata mashariti ikiwa ni pamoja na kulala ndani ya chandalua chenye dawa ,pamoja na kufukia madibwi yote basi ugonjwa huu unaweza kutoweka kabisa .
kwa upande wa wauguzi alisema kuwa amesikia kero zao na atazifanyia kazi kwa yale ambayo yatawezekana,badhi ya matatizo ya wauguzi ambayo wameyataja leo mbele ya Raisi ni pamoja na kuitaji malipo ya mazingira hatarishi ,walitaka vyeo vipandishwa kwa wakati pamoja na kulipwa malipo ya likizo kwa wakati
Pia waliomba ruzurku kwa masomo ya juu pamoja na kuboreshewa maeneo ya kazi