Huenda Saratani ya Tezi-Kibofu ni ugonjwa wa Zinaa unaosababishwa na ugonjwa wa zinaa ambao dalili zake sio wazi sana.
Hii ni kwa mujibu wa wanasanyansi nchini
Marekani. Wanasema kwamba Saratani hiyo husababishwa na maradhi fulani
ambayo huenezwa wakati wa kitendo cha ngono.
Lakini wataalamu wanasema kuwa
ushahidi bado haupo kama kweli Saratani hiyo ni moja ya magonjwa ya
zinaa na inasababishwa na magonjwa ya zinaa.
Ingawa baadhi ya Saratani husababishwa na
maradhi fulani fulani, kitengo cha utafiti wa Saratani nchini Uingereza
kinasema kuwa ni mapema mno kuongeza Saratani ya tezi kibofu kwa
Saratani hizo.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo walichunguza celi za tezi kifobu cha binadamu katika maabara.
Waligundua kuwa maradhi ya zinaa yaitwayo, 'Trichomoniasis' yalichochea ongezeko la Saratani hiyo.
Hata hivyo mfumo wa maisha pia unachangia ongezezeko la visa vya magonjwa ya Saratani.
Ugonjwa wa 'Trichomoniasis' unaaminika
kuwaathiri watu milioni 275 duniani na moja ya maradhi maarufu ya Zinaa
ambayo hayasababishwi na Virusi
'Dalili za Trichomoniasis'
Kawaida, mtu hatapata dalili za ugonjwa huo na inawezekana asijue kama anaugua ugonjwa huo.
Wanaume huhisi kujikuna sana ndani ya uume wao ,
kupata hisia za kuchomeka wakati wanapokwenda haja ndogo au kuvuja
majimaji meupe kutoka kwa uume wao.
Wanawake pia wana hisia tu sawa na hizo katika sehemu zao za isiri pamoja na kuwa na harufu mbaya.
Utafiti huu wa hivi karibuni sio wa kwanza kuhusisha ugonjwa wa 'Trichomoniasis' na Saratani ya Tezi kibofu.
Utafiti uliofanywa mwaka 2009 ulipata kuwa robo
ya wanaume walio na Saratani hio walikuwa na dalili za ugonjwa wa
Trichomoniasis na wanaume hawa pia walikuwa na uvimbe ambao ulikuwa
umekomaa mno.
'Hoja ya Uchunguzi zaidi'
Uchunguzi huo pia unaonyesha njia ambazo ugonjwa huo wa zinaa unawaweka wanaume katika hatari ya kupata Saratani ya tezi kibofu.
Profesa Patricia Johnson na watafiti wenzake,
waligundua kuwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa 'Trichomonas
vaginalis' - huvuja proteni ambayo husababisha Saratani ya Tezi Kibofu
kuzuka.
Mtaalamu wa afya, Nicola Smith,anasema uchunguzi
huu unaonyesha tu njia ambazo ugonjwa wa zinaa wa Trichomonas vaginalis
unazidisha uwezo wa mtu kuugua Saratani ya Tezi Kibofu na kuchochea
seli kukuwa kwa kasi.
"Lakini uchunguzi huu ulifanywa tu katika
maabara na matokeo ya awali kwa wagonjwa yalikosa kuonyesha uhusiano
kati ya ugonjwa huo na Saratani ya Tezi Kibofu,'' alisema Bi Nicola
Kwa kauli hii wanasema kuwa uchunguzi zaidi
unahitajika ili kuabini hasa kinacho sababisha Saratani ya Tezi kibofu
kwani ugonjwa wa Trichomoniasis husababisha tu mazinigira kwa ugonjwa
huo kukomaa ila sio chanzo cha ugonjwa wenyewe.