Mmoja
wa wakulima wa nanasi wilayani Handeni Bi Sabrina Rory Sasumua,
akionyesha aina ya nanasi lenye uzito wa kilo mbini na nusu kutoka
katika shambani lake eneo la Kwamsisi wilayani Handeni.
Afisa
Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia
akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima
wilayani humo.
Baadhi ya akina mama wa eneo la Soni katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakifanya biashara za matunda na mbogamboga.
Mkuu
wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, kulia akishika
mmoja ya mihindi katika shamba linalomilikiwa kwa pamoja na Bw. Adolf
Mpanju na Bw. Stanslaus Majura, wakati wa ziara yake ya kuangalia mazao
mashamabani katika kijiji cha Manga wilayani Handeni.
Shamba la mahindi katika kijiji cha Manga likionekana kustawi vya kutosha.
Ufugaji wa kuku wa kisasa katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga ni moja ya shughuli zinazowapatia wananchi fadhe za ziada.
Mmoja
ya wakulima wakubwa wilayani Handeni Bw. Rory Nightingale, katikati
akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu
kulia alipotembelea katika shamba hilo akiongozana na Afisa Kilimo wa
wilaya ya Handeni Bw. Yibarik Chiza kuona ana ya mananasi katika shama
hilo lililopo katika eneo la Kwamsisi wilayani humo.
Afisa
Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia
akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima
wilayani humo.
Mmoja
wa Wakulima wa Ufuta katika Kijiji cha Misima wilayani Handeni Bw.
Rashidi Dempombe, akimweleza afisa Kilimo wa wilaya hiyo Bw. Yibarik
Chiza, kwa namna alivyolima na kupanda zao hilo ambalo ni la biashara.