Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) Dr Wilbrod Slaa
(haonekani vizuri pichani) akizungumza na wananchi wa Arusha katika
viwanja vya Kilombero ikiwa ni mfululizo wa Mikutano ya Umoja wa Katiba
ya Wananchi iliyoanza juzi katika maeneo tofauti ya nchi. Katika mkutano
wa Arusha Dr Slaa aliambatana na viongozi wengine kutoka NCCR Mageuzi
na Chama Cha Wananchi (CUF) iliyowakilishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu
Bw Mustafa Mwanri.
Ulinzi
ulikuwa ni wa uhakika kutoka kwa vikosi vya vyama vyote vitatu. Pichani
ni kijana wa Redbrigade ya Chadema Bw George katika suti maridadi.
Viongozi
mchanganyiko wa vyama vyote vitatu. Katikati anaonekana Dr Slaa akiwa
kulia kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Mh Philemon Ndesamburo ambaye
amejitolea Helkopta yake pamoja na gharama za mafuta na rubani kuzunguka
Kanda yote ya Kaskazini hadi Tarime Mkoani Mara.
Kutoka kushoto, Bw Elifuraha wa ArushaMambo Radio, Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema, Mh Amani Golugwa na Dr Slaa