meneja mauzo wa PSI kanda ya kaskazini Peleatian Masai akiwa anatoa mada kwa washiriki
baadhi ya wahudumu wa vituo vya afya kutoka mikoa ya Arusha wakiwa wanafatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na PSI katika ukumbi wa Olasiti garden uliopo nje kidogo ya jiji
Mshauri wa huduma na bidhaa wa PSI Dr,Wambura Maseke akitoa mafunzo kwa washiriki katika hotel ya Olasiti
PSI Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalotoa
huduma za kiafya chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii, likimejikita
katika idara za kinga za wizara hiyo.
Katika kuhakikisha wakazi wa Arusha
wanaendelea kupata huduma bora za afya imetoa mafunzo kwa wahudumu wa
vituo vya afya vipatavyo 50 vya serikali na vile vya watu binafsi ili kuboresha
utoaji wa huduma bora za dawa za uzazi wa mpango zijulikazo kama (familia
products and services) zinazosambazwa na shirika hilo.