Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bwana Crescentius Magori
akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete katika viwanja vya AICC mjini Arusha ambapo alifungua
mkutano Mkuu wa wadau wa NSSF leo jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo muda mfupi baada ya
kuwasili katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC mjini
Arusha leo ambapo alifungua mkutano wa nne wa wadau wa NSSF.Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mages Mulongo,
Naibu Waziri wa TAMISEMI Kassim Majaliwa, Waziri wa Kazi na Ajira
Gaudencia Kabaka,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Bwana Abubakar
Rajabu na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NSSF Bwana Crescentius Magori Picha na Freddy Maro.