Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni
alipofika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, wakati wa
mahafali ya Kidato cha Sita. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mhandisi Aloyce Peter Mushi.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, Sista Anna akimpeana
mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati
wa mahafali ya Kidato cha sita yaliyofanyika Shuleni hapo. Benki ya CRDB
ilitoa msaada wa shs. milioni 5 na katika harambee iliyofanyika shuleni
hapo jumla ya sh.milioni 10 zilipatikana.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita wakiimba ngojera wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha sita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwasili Shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya wasichana ya Kibosho, Sista Anna akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kibosho, Mhandisi Aloyce Peter Mushi akizungumza wakati wa hafla ya mahafali ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Kibosho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk. Charles Kimei
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizindua jengo la mahabara ya Shule ya Sekondari
Kibosho, wakati wa mahafali ya 30 ya kidato cha sita yaliyofanyika Mkoani
Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, sista Anna na kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Mhandisi Aloyce Peter Mushi. Benki ya CRDB ilitoa mchango wa shs. milioni
5 kwa ajili ya shule hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mhandisi Aloyce Peter Mushi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Sista Anna.
Shule ya Serkondari ya Kibosho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizindua gazeti la shule.
Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, Sista
Anna na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mhandisi Aloyce Peter Mushi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa zawadi kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Kibosho wakionesha umahiri wa kufanyakazi za nyumbani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa
mahafali ya 30 ya Shule ya Sekondri ya wasichana ya Kibosho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akimkabidhi hundi ya shs.
milioni 5 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Wasichana Kibosho, Mhandisi Aloyce Peter Mushi, kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya shule hiyo.
Keki ya mahafali ya kidato cha sita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akikata keki wakati wa mahafali hayo.