Mkuu wa idara ya utalii katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Eva Mallya akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu mpya wa kuhamasisha utalii wa ndani. |
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa idara ya utalii katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro Eva Mallya (hayupo pichani) |
HIFADHI ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,imetoa fursa
kwa wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla kupanda mlima
Kilimanjaro hadi kilele cha Shira (Shira Plateu) kwa nusu bei yaani shilingi 5,000
kwa watu wazima kuanzia miaka 16 na kuendelea na Shilingi 1,000 kwa watoto
kuanzia 5-15.
Gharama hii ni nusu ya bei halisi ambayo ni shilingi
10,000 kwa watu wazima na 2,000 kwa watoto.Ofa hii inaanza Mei 15 hadi Mei 18
mwaka huu,Safari hiyo itakuwa ya kutwa nzima kwenda na kurudi siku hiyo hiyo na
usafiri utatolewa bure na hifadhi (KINAPA).
Vituo vya kujiandikishia ni mgahawa wa Fresh coach
Moshi mjini ,Hosptal ya KCMC,Njia Panda ya Himo (Stand ya Same),Bomang’ombe
(Kiwire Supermarket) na KINAPA Marangu(Mapokezi).Kazi ya uandikishaji imeanza
tayari.Vituo vitakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi.Wanaopenda kupanda
wanashauriwa kufika katika maeneo hayo tajwa.
Vituo vya kuanzia safari ni viwili Mgahawa wa Fresh
Coach Moshi mjini na Bomang’ombe (Kiwire Supermarket),Safari itaanza saa moja
kamili asubuhi.