Wanafunzi
125 wa michezo ya riadha, mpira wa miguu, pete na wavu, wa shule za sekondari
Wilaya ya Hanang’ wanatarajia kushiriki mashindano ya umoja wa michezo ya shule
za sekondari (Umiseta) Mkoani Manyara.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, mratibu wa umiseta wilayani humo, Caroline Marshali
alisema wavulana na wasichana wa shule tofauti za sekondari wanashiriki michezo
mbalimbali ya kutafuta wawakilishi wa wilaya hiyo.
Marshali
alisema wanafunzi hao wa shule za sekondari watawakilisha wilaya hiyo kwenye kuruka
juu, chini, kutupa mkuki, sahani, tufe, mbio ndefu na za mita 100, 200, 400, 800,
1,500 na mbio ndefu za marathoni.
“Pia
kutakuwa na timu za mpira wa miguu za wasichana na wavulana, mpira wa wavu na
mpira wa pete na wachezaji wetu wamejiandaa ipasavyo kwenye mashindano haya ili
kuipa sifa wilaya yetu,” alisema.
Naye,
Mwenyekiti wa umoja wa wakuu wa shule za sekondari (Tahosa) wilayani Hanang’
John Malley alisema wamewaandaa ipasavyo vijana wao ili washiriki kikamilifu
michezo hiyo na kuleta ushindi katika wilaya yao.
“Pamoja
na hayo tunamshukuru Mbunge wa jimbo letu Mary Nagu kwa kutuunga mkono kwenye
maandalizi haya ya kwenda kushiriki mashindano ya mkoa kwa ikiwemo kutupa
vyakula,” alisema Malley.
Nao
baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu, wavu na kuruka juu, Nobert Aushak, Judith
Mkilanya na Anna Aney walisema kupitia michezo wanajijenga kisaikolojia ili
wafanikiwe katika masomo yao kwani hawana hofu ya mitihani.
Walidai
kuwa zaidi kufahamiana na watu mbalimbali kupitia michezo, pia wanajenga afya
zao kwa kuwa wakakamavu na wanajiamini zaidi pindi wakiwa masomoni hivyo
wanatarajia kufanikiwa pia kimasomo.