Wakazi
wa mji wa Sikonge wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo
katika uwanja wa CCM,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alipowahutubia.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Sikonge kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,mkoani Tabora.
Katibu
wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye,akiwahutubia mamia ya wakazi
wa mji wa Sikonge waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa CCM,Wilayani humo mkoani Tabora.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la
Sikonge,Said Mkumba kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakumba
wakulima wa zao la Tumbaku wilayani Sikonge mkoani Tabora,ambapo
inaelezwa kuwa wakulima hao wamekuwa wakilaghaiwa,kudhulumiwa na
kunyonywa na vyama vya ushirika huku ubadhilifu mkubwa wa fedha
ukifanywa na vyama hivyo.
Mbunge wa jimbo la Sikonge,Said Mkumba akiwahutubia wananchi wa sikonge mkoani Tabora.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongezana na Mkuu wa Mkoa,Mh,Fatma
Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye
wakikagua mradi wa ufugaji kuku wa asili ikiwa ni sehemu ya mradi wa
Vijana wa Path Finder Green City,Wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kwenda kukagua mradi wa ujenzi wa
kituo cha afya kijiji cha Mazinge wilayani Sikonge,kituo hicho kitakuwa
kinatoa huduma mbalimbali kama vile wagonjwa wa nje,kuhudumia Wazazi na
watoto,waja wazito,sehemu ya kuhifadhia maiti,Wodi ya Wanaume na
nyinginezo.
Mkufunzi
wa Kilimo cha Tumbaku kutoka kampuni ya TLTC,Goodluck Mmasi akifafanua
namna ya uhifadhi tumbaku kwenye maghala na namna
inavyochambuliwa,Mradi huo ni wa Vijana wa PathFinder Green City,ambao
wamekuwa wakijituma kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo na za ujenzi
pia katika suala zima la kujikwamua na umasikini.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala
la Vijana wa PathFinder Green City,katika kata ya Pangale Wilayani
Sikonge mkoani Tabora.
Sehemu
ya mradi wa Vijana wa Ufugaji Nyuki katika kijiji cha Path Finder Green
City kilichopo katika kata ya Pangale,wilayani Sikonge mkoani
Tabora,Vijana hao wana jumla ya Mizinga ya nyuki 600 maalum kwa ufugaji
nyuki.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia,wakazi wa Sikonge
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,wilayani
Sikonge mkoani Tabora.Kinana alizungumzia changamoto mbalimbali
zinazowakumba wakulima wa zao la Tumbaku huku akionesha kabrasha la
taarifa ya ukaguzi na uchunguzi wa chama cha Ushirika cha WETCO
LTD,ambalo linaeleza namna wakulima wa Tumbaku walivyoibiwa mamilioni ya
fedha.
Aidha,Wananchi
wa Sikonge wameulalamikia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha uliofanywa na
viongozi wa vyama vya ushirika,Kufutia taarifa ya ukaguzi na uchunguzi
katika vyama hivyo vya ishilika,inaelezwa kuwa kiasi cha fedha milioni
28 zimefujwa,na kwamba wamekuwa wakicheleweshewa malipo ya fedha zao na
pia kutolipwa kwa wakati,jambo ambalo limekuwa likiwakera wakulima hao
na kuwarudisha nyuma katika suala zima la maendeleo.
Kinana
aliongeza kusema kuwa vyama vya ushirika vimeanzishwa kwa wingi na
wajanja wachache kwa ajili ya kujinufaisha wao na kuwanyona na
kuwadhuruma wakulima wa Tumbaku,hivyo Kinana alisema kuwa amekisikia
kilio cha wakulima hao,na ameahidi kuyafikisha malalamiko hayo kwa Rais
Jakaya Kikwete na hatimaye kupatiwa ufumbuzi.