Ticker

6/recent/ticker-posts

KESI YA BILIONEA WA MADINI YA TANZANITE UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA MASHAHIDI.

Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara bilionea wa madini ya Tanzaniete Erasto Msuya wakiingizwa mahakamani.

Na Ripota wetu , Moshi
UPELELEZI katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Erasto Msuya aliyeuwawa Agosti 07 mwaka jana, umekamilika ambapo May 20, mwaka huu, upande wa mashitaka unataarajiwa kuwasilisha taarifa za mashahidi waliyoyandika polisi (Commital Proceedings) mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mwendesha Mashitaka, Wakili wa serikali,  Florentina Sumawe, jana aliiambia mahakama  ya hakimu  mkazi mbele ya hakimu ,Munga Sabuni kuwa tayari upelelezi umeshakamilika na kwamba kinachosubiriwa ni Jalada lenye taarifa za mashahidi wa Jamhuri inayoandaliwa na Mahakama kuu kuwasilishwa mahakamani hapo.
 "Ikupendeze mheshimiwa Hakimu, kwamba Upeleelzi wa kesi hii
imekamilika, leo tulitarajia kusoma taarifa za mashahidi wa upoande wa mashitaka lakini haitakuwa hivyo kutokana na jalada hilo kuwa mahakama kuu, hivyo tunaiomba mahakama yako tukufu kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya zoezi hilo," alieleza Wakili Sumawe.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu mkazi, Munga Sabuni alisema kwa
kuzingatia taratibu za kisheria chini ya kesi za makosa ya jinai,
mahakama yake imesikiliza kwa umakini ombi la upande wa Jamhuri na hivyo basi kesi hiyo itafikishwa mahakamani hapo May 20 kwa ajili ya kutajwa.
Marehemu Erasto Msuya (43), aliuwawa kikatili Agosti 07, kwa kupigwa risasi 13, majira ya saa 6:30 mchana kando ya barabara kuu ya Arusha-Moshi, eneo la Mijohoroni,Wilaya ya Hai, Karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kufa papo hapo.
Wanaoshtakiwa 7 kuhusika ni mshtakiwa namba 1, Sharif Mohamed Athuman (31) mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Mshitakiwa Shaibu Jumanne Saidi "Mredi" (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya Simanjiro na Mussa Juma Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa mrefu mkoani Arusha.
Wengine ni  Mfanyabiashara wa madini na mkazi wa Arusha, Jalila Zuberi Said (28),mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed Jabir "Msudani" au "Mnubi"(32), mkazi wa Dar es salaam na Lang'ata Wilayani Hai na Karim Kihundwa (33) mkazi wa Kijiji cha Lawate, Wilaya ya Siha.

Post a Comment

0 Comments