BODI YA WAKURUGENZI MUWSA WATEMBELEA VYANZO VYA MAJI HIMO NA MOSHI
Posted by
woinde
on
Wednesday, May 07, 2014
in
Habari
MATUKIO
|
|
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Profesa
Faustine Bee akiwa juu ya Bomba kwa lengo la kutizama kwa
ukaribu Chemichemi hiyo . |
|
Wajumbe wakitizama
Chemichemi. |
|
Meneja rasilimali watu wa mamlaka ya maji
safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Michael Konyaki akitoa maelezo
kwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo Hajira
Mmambe.Wengine ni Meneja ufundi,Kibasa(shati nyeupe)meneja biashara
John Ndetiko(mwenye suti)na meneja Biashara kituo cha Himo
,Sanagawe(shati ya Bluu) |
|
Wajumbe wakiendelea kupatiwa
maelezo. |
|
Baada ya kutizama Chemichemi hiyo safari ya
kurudi ikaanza kama kawaida kiongozi ,Mama Shally Raymond akaongoza
safari ya kupanda kilima. |
|
Baadae wajumbe wa bodi wakatembelea matenki
ya kuhifadhia maji baada ya kusukumwa kutoka katika Chemichemi iliyoko
mto Ghona na kupatiwa maelezo toka kwa mkurugenzi mtendaji wa
MUWSA,Mhandisi Cyprian Luhemeja.. |
|
Wajumbe wa bodi wakahitimisha ziara yao kwa
eneo hilo la Himo kwa kutembelea ofisi mpya za mamlaka hiyo kituo cha
Himo. |
|
Wakiwa Moshi mjini wajumbe wa Bodi
walitembelea Chanzo kipya cha maji kilichopo mto Karanga ambacho kwa
sasa ujenzi wake unaendelea. |
|
Ziara hiyo ikahitimishwa kwa majumuisho
yaliyofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katikati ya mji wa
Moshi. |
|
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi
wa mazingira mjini Moshi,Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa taarifa
mbele ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka
hiyo. |
|
Baadaye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingra mjini Moshi,Shally Raymond
pamoja na wajumbe wengine wa bodi wakapata fursa ya kuzungumza juu ya
yale waliyoona wakati wa ziara hiyo. |
|
Baaadhi ya wajumbe wa bodi.
|
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,(MUWSA)wakiingia katika
gari tayari kwa safari ya kutembelea vyanzo vya maji
. |
|
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya
maji safi na maji taka wakielekea kwenye vyanzo vya maji
vinavyosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini
Moshi, MUWSA. |
|
Wajumbe wa bodi wakiongozwa na mwenyekiti
wao Shally Raymond (shoto)wakushuka vilima na kuluka vijito hatimaye
wakafika mto Ghona katika mji mdogo wa Himo ambako kuna chemichemi ya
maji inayotumika kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo la
himo. |
| |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia