JESHI la
Polisi mkoani Manyara, linawashikilia watu watano kwa makosa tofauti,
likiwemo la Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari
Chief Sarwati, akiwa na Bastola moja aina ya Chines iliyofutwa namba za
usajili pamoja na risasi 6 zikiwa ndani ya magazine kinyume cha sheria
Akithibitisha
kutokea kwa matukio hayo leo Mei 16, 2014, Kamanda wa Polisi mkoani
humo, Deusdedit Nsimeki, amesema katika tukio la kwanza lilitokea Mei
14,2014 ambapo Polisi walimkamata, Said Shabani (16) mwanafunzi wa
kidato cha pili katika shule hiyo, na Lutemba John (22) mkazi wa mkoa wa
Kigoma wakiwa na silaha hiyo kinyume na sheria.
Nsimeki,
amesema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walikamatwa kwenye gari namba T.
313 ALZ, Rosa mali ya Laurent Sule, ambapo gari hilo hutumika
kusafirisha abiria toka Mbulu kwenda Hydom.
“Hawa
tutaendelea nao kwa mahojiano kuhusiana na hiyo Bastola na risasi
husika na kujua walikuwa wanaenda wapi, kwani kutokana na taarifa za
awali zinasema kwamba walikuwa wanaenda kufanya ujambazi huko Hydom”
alisema Nsimeki.
Amesema
katika tukio lingine lilitokea Mei 15, 2014 saa tisa alfajiri maeneo ya
Himiti, ambapo wananchi wapatao 30 wakiongozwa na Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Idd Hassan, (53) wakiwa kwenye msako waliwakamata watu wanaovua
samaki ndani ya Ziwa Babati kwa kutumia sumu, wakati ziwa hilo likiwa
limefungwa na Serikali ya mkoa.
“Ilipofika
muda huo, wananchi kwa kushirikiana na mwenyekiti huyo pamoja na Askari
Polisi, tulifanikiwa kukamata watu watatu ambao walikuwa wanafanya
shughuli hiyo katika Ziwa Babati kinyume na taratibu na sheria, alisema
Nsimeki.
Amewataja
watuhumiwa hao kuwa ni, Athuman Rashid (32), Halifa Hussein (28), na
Hassan Hamis (33) ambao kabla ya kufikishwa ufukweni walijirusha Kwenye
Ziwa hilo na kufanikiwa kutoroka.
Amesema
katika msako huo, waliweza kukamata samaki kilo 60, nyavu moja pamokja
na dawa aina ya DAZBAN iliyotumika kuua/kuvua samaki hao, ambapo kwa
mujibu wa taarifa hiyo inasadikiwa dawa hiyo kwenye maduka ya pembejeo
za kilimo.