meneja wa usambazaji wa kada ya
kaskazini wa PSI Tanzania ndugu Pelestian Masai,akiwa anatoa mada katika mafunzo hayo
wasambazaji wa kondom pamoja na wakufunzi kutoka PSI wakiwa katika picha ya pamoja
Shirika afya lisilo la
kiserikali linalo fanya kazi chini ya wizara ya afya PSI/Tanzania kanda
ya kaskazini ambalo ni wasambazaji wa salama kondom na bidhaa nyingine
za afya zikiwezo zile za uzazi wa mpango za familia pamoja watergurad,
mwishoni mwa wiki limefanya mkutano na mawakala wateule wa kanda ya
kaskazini inayohusisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha an Manyara
uliofanyika katika hoteli ya Silver Palm iliyoko hapa jijini Arusha
ukiwa na lengo la kujadili mafanikio, changamoto na kuweka mikakakati ya
kufanikisha na kuimarisha usambazaji wa bidhaa hizo kwa kanda ya
kaskazini.
Akizungumzia
hali ya usambazaji wa salama kondom meneja wa usambazaji wa kada ya
kaskazini wa PSI Tanzania ndugu Pelestian Masai, amesema mpaka sasa PSI
kanda kwa kushikirikiana vema na wadau wake na wamefanikiwa kusambaza
salama zaidi ya Kondom milioni 9 katika mikoa hii minne ambapo lengo kwa
mwaka huu ni kufikia condom zaidi ya milioni 20, wakati jiji la Arusha
pekee kwa mwaka 2014 ndilo linaongoza likiwa limesambaziwa zaidi ya
condom milioni 5 kwa mwaka huu pekee.
lengo
likiwa ni kusaidia juhudi za serikali katika jitihada za kupambana na
mambukizi ya ukimwi, magonjwa ya ngono pamoja na kuboresha huduma za
uzazi wa mpango.