MEMBE ATEMBELEA UTURUKI KIKAZI


Waziri Mkuu wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Ankara, Uturuki
Mazungumzo yanaendelea kati ya Waziri Mkuu wa Uturuki (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania. Mwingine katika picha ni Bibi Victoria Mwakasege, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Waziri Membe kulia akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Uturuki mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo. 
Mazungumzo kati ya Waziri Membe na Waziri na Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki 
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyevaa shati la njano kulia ukiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Uturuki unaongozwa na Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Emrullah Isler wa tatu kutoka kushoto
Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard K. Membe akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki
Waziri Membe naye akimpa zawadi ya kinyago Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki 
Mhe. Membe na Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki wakijadili suala baada ya zoezi la kukabidhiana zawadi kukamilika Mazungumzo ya Waziri Membe na Wazri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe wa tatu kutoka kushoto na ujumbe wakijadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano na Uutruki na ujumbe wa Uturuki unaonekana katika picha ya chini.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Almet Dovutoglu wa pili kutoka kulia akiwa na ujumbe wake wakati wa mazungumzo na Mhe. Membe. Mkutano na Waandishi wa Habari
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe akihutubia Mkutano wa Waandishi wa Habari huku akimshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Almet Dovutoglu
Waziri Membe akiendelea kuwahutubia waandishi wa habari hawapo pichani Mapokezi ya Mhe. Membe nchini Uturuki
Waziri Membe akipeana mikono na watu waliofika Uwanja wa Ndege wa Ankara kumpokea

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post