Baadhi
ya viongozi wa dini kutoka katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwasili
katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini
Thailand. Viongozi hao walifanya ziara nchini humo kwa ajili ya
kujifunza na kupata uzoefu wa uendelezaji wa sekta ya gesi.
Viongozi
wa dini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili Uwanja wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Bw.
Mohamed Sinani akielezea jinsi nchi ya Thailand ilivyopiga hatua
kimaendeleo kutokana na mchango wa sekta ya gesi.
Badhi ya viongozi wa dini wakiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kutokea nchini Thailand.
Padri
Dkt. Aidan Msafiri ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Agustino tawi la Mtwara akizungumza na waandishi wa habari
katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) mara baada ya
kuwasili kutoka nchini Thailand.
Makamu
wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kutoka dayosisi ya
Newala Bw. Oscar Stephen akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake
uzoefu walioupata walipokuwa nchini Thailand hususan katika sekta ya
gesi.
Shehe
Mkuu kutoka Mkoa wa Mtwara Bw. Nurdin Abdalah akiwaeleza waandishi wa
habari jinsi wananchi wa Thailand walivyoweza kutunza vyema rasilimali
yao ya gesi ikiwa ni pamoja na usimamizi wa sekta nyingine.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdallah Hamis Ulega akizungumza na waandishi wa
habari jinsi wananchi wa Thailand walivyonufaika na rasilimali ya
gesi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia