Huyu ndio Redd's Miss Hai 2014, Neeema Swai.
Upande wa kushoto ni muwakilishi kutoka
TBL akimkaribisha mgeni rasmi ili aweze kufungua mashindano ya Redd's
Miss Hai 2014. Ambapo mgeni rasmi alikuwa ni hakimu wa wilaya ya Hai
Bwana Dennis ambae alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Hai ambaye
alishindwa kufika.
Warembo wa Redd's Miss Hai 2014 wakitoa burudani.
Warembo wa Redd's Miss Hai 2014 wakiwa katika vazi la jioni.
Warembo wa Redd's Miss Hai 2014 wakiwa katika vazi la ufukweni.
Baada ya mchujo walibakia walimbende watano kati ya kumi na mmoja waliokua kwenye kinyanganyiro hicho.
Mshindi wa tatu, Redd's Miss Hai 2014 ni Navia Samwel, na mrembo huyu ndie aliyefanikiwa kunyakua taji la Miss talent wilaya ya Hai.
Huyu nimshindi wa pili, Redd's Miss Hai 2014, Neema Lema.
Aliyefanikiwa kunyakua taji la Redd's Miss Hai 2014, ni Neeema Swai.

Huyu ndie mlimbende aliyenyakua taji la Miss talent katika wilaya ya Hai, Navia Samwel ambaye pia ni mshindi wa tatu.

Jaylone
ni msanii ambaye leo nyota yake imeweza kung'aa sana kwa kukubalika na
mashabiki pamoja na kutunzwa na pesa nyingi kuliko kawaida..
Wakati
Jaylone anaimba shabiki mmoja anayefahamika kama Dullah Boy (aliyevaa
kamtula na kofia nyeusi) alipanda jukwaani na kitita cha pesa na kuanza
kumrushia Jaylone zaidi ya lakini mbili za kitanzania kitendo ambacho
kiliwashangaza watu wote waliokuwa ukumbini hapo.

Babi D'e Conscious akiwa na Mohamed Waziri maarufu kama Dj Virus.
Swala la ulinzi na usalama pia lilikuwa vizuri sana.