Warembo wanaowania taji la Miss Dar City Center 2014 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa Habari hii leo.
Mratibu wa shindano hilo, Judith Michael akizungumza na wanahabari, pamoja nae ni Mkufunzi wa warembo hao.
WANYANGE 20 wanao wania taji la Miss Dar City Center kesho Mei 16 mwaka huu watawasha moto vikali katika ukumbi wa Maisha Clab wakati wa shindano lao la Vipaji.
Shindano hilo litaongozwa na wasanii, Rich Mavoko,
Bonge la Nyau na TID ‘Mnyama’ wanataraji kuwaongoza warembo hao kuwania taji la Vipaji 'Miss Talent Dar City Center 2014."
Akizunguumza na
waandishi wa Habari Dar es Salaam leo mratibu wa Shindano hilo, Judith Michael Amesema
warembo wote 20 wapo katika hali nzuri na wamejifua vya kutosha kwaajili ya
shindano hilo la vipaji.
“Tunaamini shindano la
mwaka huu litakuwa zuri sana warembo wamejiandaa vya kutosha, tunapenda
kwaalika wadau mbalimbali wa masuala ya urembo waje kwa wingi Club Maisha siku
hiyo ya Ijumaa ili waweze kushuhudia wenyewe jinsi warembo wa jiji letu
walivyojaliwa vijapaji hakika miss Tanzania yupo Dar City Centre,” alisema
Judith.
Aidha Judith amesema
shindano la Miss Dar City Centre litafanyika Mei 24 mwaka huu katika ukumbi wa Escape
One Mikocheni ambapo pia ameahidi shindano hilo kuwa la aina yake.
Judith amewataja warembo
wanao wania taji hilo kuwa ni pamoja na Naomy Kisaka, Nasreen Abdul, Gladys Matson, Habiba Israel, Jenny
Zahn,
Doreen Elias, Winniefrida Msusa, Grace Mella na Rehema Athumani.
Wanyange wengine ni Francisca
Simon, Salha Suleiman, Dorica Daud, Agriphina Yelezwa, Sabina Thomas, Jihan
Dimachk, Aziza Thabiti, Hatma Rshidi Nyembo na Neema Sisamo.
Huku wadhamini wa
Shindano hilo la Miss Dar City Centre ni Prima Total Hair Collection,Gumbo Investment
Diamond Bureau Dechange, Father Kidevu Blog, Maisha Club,Q Plus, Zanzi Cream, Clouds
Fm, Machapta, Flamour Cosmetics, Valley Spring, Best Point Hotel, Atik Aluminium,
Jambo Leo, Blog Ya Wananchi na Skylight Band.