Sehemu ya kwanza kabisa kuiona unapopanda mlima Kilimanjaro ni misitu uliotokana na kupandwa kwa miti inayotumika kwa ajili ya utengenezaji wa Mbao. |
Baadae unaicha hiyo misitu kisha unakutana na uoto wa asili wa miti mifupi . |
Kadri unavyo panda juu hali ya uoto inabadirika na hatimaye kukutana na nyasi fupi fupi iliyojishikiza kwenye miamba. |
Kwa watali wa ndan sasa wanaweza tumia barabra maalum kupanda na magari yao kwenda kujionea mandhari ya mlima Kilimanjaro ukiwemo uoto huo wa asili na miamba. |
Maua ya aina mbalimbali yanapendezesha maeneo hayo. |
Hali ya hewa katika maeneo hayo hubadilika kila baada ya dakika kadhaa,wakati mwingine mnaweza msionane. |
Wakati mwingine hali ni nzuri sana unatizama kila pembe ya mlima. |
Mawe yaliyotokana na kurushwa kwa uji uliotokana na Volcano. |
Maumbile mbalimbali ya vilima vilivyosalia kutokana na volcano hiyo. |
Hali ya hewa inabadilika pole pole kila eneo utakalo pita. |
Mabonde makubwa yaliyoambatana na mito kutoka katika miinuko ya mlima. |
Viwanja vya ndege aina ya Helcopter katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uokoaji kwa watalii wanaopata matatizo. |