HAATIMAYE MWENGE WA UHURU WAWASHWA RASMI JANA MKOANI KAGERA,TAYARI KUKIMBIZWA KATIKA WILAYA 127


 Makamu wa Rais wa, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera jana.
 Wakimbiza Mwenge kitaifa wakikimbiza Mwenge wa Uhuru kuelekea nje ya Uwanja wa Mpira wa Kaitaba tayari kuanza ziara ya kukagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispa ya Bukoba.
 Watu mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.
 Watoto wa Haraiki wakionyesha michezo mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo mjini Bukoba.
Baadhi ya watoto wakifuatilia matukio mbalimbali wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru bila kujali mazingira yaliyopo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post