Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na
matumizi ya
fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri
Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi,
35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni
za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi.
Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari wakifuatilia Hotuba hiyo.
Baadhi
ya wadau wa Habari akiwepo Mkurugenzi wa Kituo cha Redio 5 cha jijini
Arusha Francis Robert (kushoto) akifuatilia hotuba hiyo bungeni mjini
dodoma leo.
Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akifuatilia mjadala wa Bajeti bungeni mjini Dodoma.
Wadau mbalimbali wa sanaa, Michezo na Utamaduni walikuwepo.
Wasanii wakifuatilia mjadala wa bajeti Bungeni, mtaalm Dude na kule P Funks mwaandaaji wa muziki na pia msaani wa muziki.