Walimbwende
15 wa Wilaya za Babati, Simanjiro, Hanang’ Mbulu na Kiteto, wanatarajia
kushiriki kinyanganyiro cha kumsaka mnyange wa mkoa huo kwa mwaka 2014, kitakachofanyika
May 31 mjini Babati.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, mratibu wa kampuni ya Mirerani Entertainment ya
mjini Babati, Akon Clement, ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo alisema
maandalizi ya mtanange huo yanaendelea vizuri.
Clement
alisema hivi sasa maandalizi ya kufanyika kwa Miss Manyara, yanaendelea vizuri
kwani washiriki kutoka kwenye wilaya hizo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya
kupatikana kwa wawakilishi wa mkoa huo.
“Tupo
kwenye mazungumzo na baadhi ya waadhamini waliotuahidi kutuunga mkono kwenye
Missi Manyara 2014, kwani mdhamini mkuu ni kampuni ya Tanzania Breweries kupitia
kinywaji chake cha Redds,” alisema Clement.
Alitaja
baadhi ya wadhamini wanaotarajia kudhamini Miss Manyara 2014 ni Manyara
Compyuta, Chuo kikuu huria Manyara, Motel Silver, Trimas Saloon,
, Shambani Solution Green belt na Fear Deal.
“Wadhamini
wengine wanaotarajia kutudhamini kwenye shindano letu ni Motel Silver, Tina
Classic, Pole pole Coach, San Abima Classic, Alno Technology, Ziggy Supermarket
na Code Marketing,” alisema Clement.
Alitoa
ombi kwa wazazi na walezi wa wilaya za mkoa huo, kuwapa ruhusa mabinti wao ili
waweze kushiriki mashindano hayo, kwani mabinti wa jamii za wairaqw, wadatoga,
wamasai, wambugwe na wafyomi wana uzuri wa asili.
“Pia
tunaendelea na mazungumzo na baadhi ya wasanii wakubwa wa muziki kutoka jijini
Dar es salaam na wasanii wengine chipukizi wa hapa hapa Babati na mkoa mzima wa
Manyara kwa ujumla watashiriki,” alisema Clement.
Tags
matukio burudani