Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), Naibu Waziri wa Fedha ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mh. Mwigulu Nchemba wakiwa kwenye boda boda, wakati wa msafara wa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika eneo la viwanja vya People’s Club mjini Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana , sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,wakiwasili kwenye viwanja vya People’s Club kwenye mkutano wa hadhara kwa staili ya aina yake kwa kutumia usafiri wa Bajaji.
Katibu mkuu wa CCM , Kinana, (kwanza kulia),akifurahia ujumbe ulioandikwa kwenye bango la wajasiriamali waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa kwanza kushoto) akishiriki kutoa burudani kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana,kuzungumza na wakazi wa jimbo la Singida mjini.
Naibu waziri wa fedha Adamu Malima,(wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na mbunge wa jimbo la Singida mjini juzi kwenye hafla ya mbunge Dewji kukabidhi msaada mabati na mifuko yenye thamani ya zaidi ya shilingi 125 milioni.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akiwa na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Kepteni John Chiligati wakiwapungia wananchi mikono kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadgara kwenye viwanja vya Peoples Club mjini Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Singida wakati wa mkutano wa hadhara kwenye viwanja hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk, Parseko Kone akizungumza kwenye Mkutano huo.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Singida,waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya peoples klabu mjini hapa.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tzeba akihutubia wananchi wa Singida mjini na kuwambia tatizo la usafiri wa treni limepatiwa ufumbuzi wa kudumu kwani Reli ya kati inaboreshwa na tayari vichwa 40 vya treni vitaanza kazi ifikapo Januari hivyo gharama za usafiri wa treni kwa abiria na mizigo itashuka.
Naibu katibu mkuu CCM taifa Mwigullu Nchemba, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya people klabu mjini Singida.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gulam Dewji,akizungumza kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi kabla hajakabidhi msaada wa Mabati na Saruji mwenye thamani ya zaidi ya shilingi 125 kwa ujenzi wa misikiti na makanisa.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Gulam Dewji ( kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati na mfuko wa saruji yaliyotoa kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa misikiti na makanisa jimbo la Singida mjini.
Naibu waziri wa maji,Amossi Makala,(wa kwanza kulia),mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Dewji,mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki,John Chiligati,mjumbe wa mkutano mkuu NEC taifa CCM manispaa ya Singida.Hassan Mazala,naibu waziri wa fedha,Adamu Malima,wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa ,Abdulrahman Kinana (katikati), Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini MO wakiteta jambo kabla ya kukabidhi misaada ya saruji na Mabati kwenye taasisi za dini jimboni humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk, Parseko Kone akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Adamu Malima, sambamba na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapten John Chiligati.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Matha Mlata, akiangalia picha mbalimbali kutoka kwa mmoja wa wapiga picha walikuwemo kwenye mkutano huo,sambamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.
“Sikia jambo Moja Mh, Wasira, mimi hapa jimboni kwangu nimefanya mambo mengi sana na wananchi wananikubali vipi kule kwako, jimboni kwako? Maneno ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini. Mohammed Dewji (MO).
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk, Parseko Kone akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Kinana,kuhusu maendeleo ya Mkoa huo, katikati ni Naibu Waziri wa Fedha na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Qeen Mlozi.
Gari la Katibu Mkuu wa CCM,Kinana likiondoka kwenye mkutano huo.
MO akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wind East Africa, Bw.Rashid Shamte mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya People's Klabu mjini Singida.
Mdau Rahim Zamunda (kulia) akifurahi kwenye picha ya pamoja na Mh. Mohammed Dewji.